登入
Yakobo 2
SRB37

Yakobo 2 (Swahili SRB 37)

1Ndugu zangu, msiwaze kwamba: Kumtegemea Bwana wetu mtukufu Yesu Kristo hupatana na kupendelea watu! 2Ni hivyo: mle mkutaniamo mkiingia mtu mwenye pete za dhahabu vidoleni, aliyevaa mavazi mazuri, tena mkiingia hata maskini mwenye mavazi machakavu, 3nanyi mkamtazama yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia: Wewe kaa hapa pazuri! kisha mkamwambia yule maskini: Wewe simama huko au kaa hapa chini miguuni pangu! 4je? Hivyo mioyo yenu haikujiumbua kwamba: Mkiwagawanya hivyo mmefuata mawazo mabaya? 5Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa! Mungu hakuwachagua walio maskini ulimwenguni, wawe wenye mali kwa kumtegemea, tena wautwae ufalme, aliowaagia wampendao, uwe urithi wao? 6Lakini ninyi mmemnyima maskini heshima. Wenye mali sio wanaowaendea ninyi kwa nguvu? Sio wanaowaburura bomani? 7Nao sio wanaolitukana lile Jina zuri, mwitwalo nalo? 8Kweli, mkilitimiza Agano la kifalme, kama lilivyoandikwa kwamba: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe! mnafanya vizuri. 9Lakini mkiwapendelea watu mnakosa, mkajulishwa na hilo agizo waziwazi kuwa wenye kulipita. 10*Kwani mtu akiyashika Maonyo yote akalikosea moja tu, amekwisha kuyakosea yote. 11Kwani yeye aliyesema: Usizini! ndiye aliyesema: Usiue! Nawe usipozini, lakini unaua, basi, umekwisha kuwa mwenye kuyapita Maonyo. 12Semeni, tena fanyeni hivyo, kama watu wafanyavyo watakaohukumiwa kwa Maonyo yanayotupatia kukombolewa! 13Kwani mtu akosaye huruma atapata naye hukumu ikosayo huruma; lakini huruma hushangilia nako kwenye hukumu. 14Ndugu zangu, mtu akisema: Niko na kumtegemea Mungu, lakini matendo hanayo, inamfaliaje? Kumtegemea Mungu kunaweza kumwokoa? 15Kwetu kukipatikana ndugu mume au mke walio wenye uchi na wenye kukosa chakula cha siku moja tu, 16mtu wa kwenu akawaambia: Nendeni na kutengemana, mwote moto, mpate kushiba! asiwape yaipasayo miili yao, itawafaliaje? 17Hapo mwaona: Kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo yakupasayo kumekwisha kuangamika kwenyewe.* 18Labda yuko atakayesema: Wewe uko na kumtegemea Mungu, nami niko na matendo; nionyesha, unavyomtegemea Mungu pasipo matendo! kisha nami nitakuonyesha, matendo yangu yanavyotimilika katika kumtegemea Mungu. 19Wewe unaamini, ya kuwa Mungu ni mmoja tu? Ni vizuri; pepo nao huyaamini hayo, lakini hutetemeka! 20Mtu mpuzi, unataka kutambua, ya kuwa kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo ni kwa bure? 21Baba yetu Aburahamu hakupata wongofu kwa matendo alipompeleka mwana wake Isaka, awe ng'ombe ya tambiko? 22Unaona: Kumtegemea Mungu husaidiana na matendo yakupasayo; napo, alipofanya yampasayo, ndipo, kumtegemea Mungu kulipotimilika kwake, 23nayo yaliyoandikwa yakatimia kwamba: Aburahamu alimtegemea Mungu, kwa hiyo akawaziwa kuwa mwenye wongofu, akaitwa mpenzi wake Mungu. 24Mnaona: Mtu hupata wongofu kwa matendo, siko kwa kumtegemea Mungu tu. 25Tena je? Yule mke mgoni Rahabu hakupata wongofu naye kwa matendo, alipowafikiza wale wajumbe na kuwatoa mjini kwa njia nyingine? 26Kwani kama mwili unavyokufa, usipopumua, vivyo hivyo nako kumtegemea Mungu kusikoendelea na matendo kunakufa.