Malaki 4 (Swahili SRB 37)
1*Kwani mtaiona hiyo siku, ikija na kuwaka moto kama wa tanuru; ndipo, waliomsahau Mungu nao wote waliofanya maovu watakapokuwa makapi, siku hiyo ijayo itakapoyateketeza, isisaze wala mizizi wala matawi yao hao; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema. 2Lakini ninyi mliogopao Jina langu jua la wongofu litawachea, nalo litakuwa linao uponya mabawani mwake; ndipo, mtakapochezacheza kama ndama watokao zizini. 3Nao wasiomcha Bwana mtawaponda na kuwakanyagakanyaga, kwani watageuka kuwa uvumbi chini ya nyayo za miguu yenu siku hiyo, nitakayoifanya mimi. 4Yakumbukeni Maonyo ya mtumishi wangu Mose, niliyomwagiza kule Horebu, awafundishe Waisiraeli wote maongozi na maagizo. 5Na mwone, nikimtuma mfumbuaji Elia kuja kwenu, siku kubwa ya Bwana iogopeshayo itakapokuwa haijatimia bado. 6Yeye ndiye atakayeigeuza mioyo ya baba, warudi kwa watoto, nayo ya watoto, warudi kwa baba zao, nisije kuipiga nchi na kuiapiza.*

