लग इन गर्नुहोस्
Hesabu 33
SRB37

Hesabu 33 (Swahili SRB 37)

1Hizi ndizo safari za wana wa Isiraeli, vikosi vyao vilipotoka katika nchi ya Misri, wakiongozwa na Mose na Haroni. 2Mose akaziandika hizo safari zao, kama walivyotoka na kuondoka kwa kuagizwa na Bwana, nayo haya ndiyo matuo yao, walipoondoka kwendelea katika safari zao: 3siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, ndiyo siku ya pili ya Pasaka, ndipo, wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi machoni pao Wamisri wote kwa nguvu za mkono uliotoka juu. 4Nao Wamisri walikuwa wakiwazika wana wao wote wa kwanza, Bwana aliowapiga kwao, kwani Bwana aliihukumu miungu yao. 5Wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi wakapiga makambi Sukoti. 6Walipoondoka sukoti wakapiga makambi Etamu ulioko kwenye mapeo ya nyika. 7Walipoondoka Etamu wakarudi Pi-Hahiroti unaoelekea Baali-Sefoni, wakapiga makambi mbele ya Migidoli. 8Walipoondoka mbele yake Hahiroti wakapita katikati ya bahari, wakaingia nyikani; walipokwenda safari ya siku tatu katika nyika ya Etamu wakapiga makambi Mara. 9Walipoondoka Mara wakafika Elimu; nako huko Elimu kulikuwa na visima vya maji 12 na mitende 70; kwa hiyo walipiga makambi huko. 10Waalipondoka Elimu wakapiga makambi kwenye Bahari Nyekundu. 11Walipoondoka kwenye Bahari Nyekundu wakapiga makambi nyikani kwa Sini. 12Walipoondoka nyikani kwa Sini wakapiga makambi Dofuka. 13Walipoondoka Dofuka wakapiga makambi Alusi. 14Walipoondoka Alusi wakapiga makambi Refidimu; huko ndiko, watu walikokosa maji ya kunywa. 15Walipoondoka Refidumu wakapiga makambi nyikani kwa Sinai. 16Walipoondoka nyikani kwa Sinai wakapiga makambi kwenye Makaburi ya Uchu. 17Walipoondoka kwenye Makaburi ya Uchu, wakapiga makambi Haseroti. 18Walipoondoka Haseroti wakapiga makambi Ritima. 19Walipoondoka Ritima wakapiga makambi Rimoni-Peresi. 20Walipoondoka Rimoni-Peresi wakapiga makambi Libuna. 21Walipoondoka Libuna wakapiga makambi Risa. 22Walipoondoka Risa wakapiga makambi Kehelata. 23Walipoondoka Kehelata wakapiga makambi mlimani kwa Seferi. 24Walipoondoka mlimani kwa Seferi wakapiga makambi Harada. 25Walipoondoka harada wakapiga makambi Makeloti. 26Walipoondoka Makeloti wakapiga makambi Tahati. 27Walipoondoka Tahati wakapiga makambi Tara. 28Walipoondoka Tara wakapiga makambi Mitika. 29Walipoondoka Mitika wakapiga makambi Hasimona. 30Walipoondoka Hasimona wakapiga makambi Moseroti. 31Walipoondoka Moseroti wakapiga makambi kwa wana wa Yakani. 32Walipoondoka kwa wana wa Yakani wakapiga makambi Hori-Hagidigadi. 33Walipoondoka Hori-Hagidigadi wakapiga makambi Yotibata. 34Walipoondoka Yotibata wakapiga makambi Aburona. 35Walipoondoka Aburona wakapiga makambi Esioni-Geberi. 36Walipoondoka Esioni-Geberi wakapiga makambi nyikani kwa Sini, ndio Kadesi. 37Walipoondoka Kadesi wakapiga makambi mlimani kwa Hori kwenye mwisho wa nchi ya Edomu. 38Ndipo, mtambikaji Haroni alipopanda mlimani kwa Hori kwa kuagizwa na Bwana, akafa huko siku ya kwanza ya mwezi wa tano katika mwaka wa arobaini tangu hapo, wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri; 39naye alikuwa mwenye miaka 123, alipokufa mlimani kwa Hori. 40Ndipo, Aradi, mfalme wa Kanaani, aliposikia, ya kuwa wana wa Isiraeli wanakuja; maana alikaa upande wa kusini wa nchi ya Kanaani. 41Walipoondoka mlimani kwa Hori wakapiga makambi Salmona. 42Walipoondoka Salmona wakapiga makambi Punoni. 43Walipoondoka Punoni wakapiga makambi Oboti. 44Walipoondoka Oboti wakapiga makambi Iye-Abarimu mpakani kwa Moabu. 45Walipoondoka huko Iyimu wakapiga makambi Diboni wa Gadi. 46Walipoondoka Diboni wa Gadi wakapiga makambi Almoni-Dibulataimu. 47Walipoondoka Almoni-Dibulataimu wakapiga makambi milimani kwa Abarimu kunakoelekea Nebo. 48Walipoondoka milimani kwa Abarimu wakapiga makambi kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili. 49Huko Yordani ndiko, walikopiga makambi kutoka Beti-Yesimoti mpaka Abeli-Sitimu kwenye mbuga za Moabu. 50Bwana akamwambia Mose huko kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, kwamba: 51Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapouvuka Yordani kuingia katika nchi ya Kanaani. 52sharti mwafukuze mbele yenu wenyeji wote wa nchi hiyo, kisha myaharibu mawe yao yote yenye machorochoro ya kuyaangukia, navyo vinyago vyao vyote vilivyoyeyushwa sharti mviharibu, napo pao pote pa kutambikia vilimani sharti mpabomoe. 53Kisha mtaichukua hiyo nchi, mkae huko, kwani nimewapa ninyi nchi hiyo, mwichukue, iwe yenu. 54Nayo nchi mtaigawanyia ndugu zenu kwa kupiga kura; ndugu walio wengi mwagawie fungu kubwa zaidi kuwa lao, nao walio wachache mwagawie fungu lililo dogo kidogo kuwa lao. Huko, kura itakakomwangukia kila mtu, kutakuwa kwake; sharti mgawiane mafungu yenu kwa mashina ya baba zao. 55Lakini msipowafukuza mbele yenu wenyeji wa nchi hiyo, basi, hao mtakaowasaza watakuwa miiba machoni penu na machomo mbavuni penu, wawasonge ninyi katika nchi, mtakayoikaa ninyi. 56Mwisho utakuwa, niwafanyizie ninyi yaleyale, niliyoyawaza kuwafanyizia wao.