Zaburi 3 (Swahili SRB 37)
1Bwana, tazama, jinsi walivyo wengi wanaonisonga! Tena ni wengi wanaoniinukia. 2Ndio wengi wanaoiwazia roho yangu ya kwamba: Hapana wokovu, atakaoupata kwake Mungu. 3Lakini wewe Bwana, u ngao inikingiayo, kwa kuwa utukufu wangu utakikweza kichwa changu. 4Ninapoipaza sauti yangu, ifike kwake Bwana, huniitikia toka mlimani kwenye utakatifu wake. 5Mimi nililala usingizi, kisha nikaamka, kwani mwenye kunishikiza ni Bwana. 6Ijapo, watu wawe maelfu na maelfu, siwaogopi, wakija kunipangia na kunizunguka. 7Inuka, Bwana! Niokoe, Mungu wangu! Kwani walio adui zangu unawapiga makofi wote, ukawavunja meno wasiokucha, wewe. 8Kwako Bwana uko wokovu, uwapatie mema wao walio ukoo wako.

