Zekaria 3 (Swahili SRB 37)
1Kisha akanionyesha mtambikaji mkuu Yosua, akisimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Satani alikuwa amesimama kuumeni kwake kumsengenya. 2Bwana akamwambia Satani: Bwana na akukemee wewe, Satani! Yeye Bwana aliyeuchagua Yerusalemu, uwe mji wake, na akukemee wewe! Kumbe huyu si kijinga kilichopona kwa kuokolewa motoni! 3Naye Yosua alikuwa amevaa nguo chafu aliposimama mbele ya malaika. 4Kisha huyu akasema na kuwaambia waliosimama mbele yake kwamba: Mvueni hizi nguo chafu! Akamwambia: Tazama, manza, ulizozikora, nimeziondoa kwako, nikakuvika nguo za sikukuu. 5Kisha akasema: Mfungeni kilemba kilichotakata kichwani pake! Wakamfunga kilemba kilichotakata kichwani pake pamoja na kumvika zile nguo, naye malaika wa Bwana alisimama papo hapo. 6Kisha malaika wa Bwana akamshuhudia Yosua kwamba: 7Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kama utakwenda katika njia zangu na kuutumikia utumishi wangu, ndipo, wewe utakapoitunza Nyumba yangu na kuzilinda nyua zangu, kisha nitakupatia njia ya kufika kwangu katikati yao hawa wanaosimama hapa. 8Sasa sikia, wewe mtambikaji mkuu Yosua pamoja na wenzako wanaokaa mbele yako, kwani ndio watu wa kutazamiwa: Mtaniona, nikimleta mtumishi wangu Chipukizi. 9Kwani tazameni: Jiwe hili, nililoliweka mbele yake Yosua, macho saba yanalielekea jiwe hili moja; tena tazameni: Mimi ninachora humo machoro yanayolipasa, kisha nitaziondoa manza za nchi hii katika siku moja; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi. 10Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Siku hiyo ndipo, watakapoalikana mtu na mwenziwe kuja kukaa pamoja chini ya mzabibu na chini ya mkuyu.

