Hosea 3 (Swahili SRB 37)
1Bwana akaniambia: Nenda tena kumpenda mwanamke mzinzi anayependwa na mwingine, kama Bwana anavyowapenda wana wa Isiraeli, nao huigeukia miungu mingine kwa kuyapenda maandazi ya zabibu. 2Nikamnunua, awe wangu, nikatoa fedha kumi na tano na frasila kumi na tano za mawele. 3Nikamwambia: Siku nyingi utakaa tu kwangu, usizini, wala usiwe wa mume; mimi nami nitakuwa vivyo hivyo kwako. 4Kwani wana wa Isiraeli watakaa siku nyingi pasipo mfalme wala mkuu, pasipo tambiko wala kinyago, pasipo vazi la mtambikaji wala Patakatifu. 5Kisha wana wa Isiraeli watarudi, wamtafute Bwana Mungu wao na Dawidi, mfalme wao; siku zitakazokuwa za mwisho watamwendea Bwana na wema wake kwa kutetemeka.

